Baba Diamond Kukatwa Miguu Kutokana na Kansa Ya Ngozi
Baba mzazi wa staa wa Bongo fleva Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Juma amedaiwa kuwa katika hai mbaya itakayompelekea kukatwa miguu katika siku za usoni.
Baada ya kujionea baba Diamond akiwa anasumbuliwa na tatizo la kansa ya ngozi, Gazeti la Ijumaa Wikienda lilimpigia simu daktari Godfrey Charle wa jijini Dar alipoelezwa kuhusu tatizo hilo, alisema kuna mambo ya kufanya ili kumnusuru kwani tofauti na hapo basi huenda akalazimika kukatwa miguu.
Kwa baba Diamond sambamba na kutibiwa kansa anatakiwa atibiwe pia maambukizi mbalimbali yanayojitokeza kwani hayo ndiyo yanasababisha mgonjwa kukatwa mguu au kiungo chochote kilichoathirika na siyo kansa.
Kwa kweli kwa hatua ile aliyofikia kupona kwake ni asilimia 50 tena kwa msaada wa ndugu yaani kama ndugu zake watamsaidia katika matibabu hivyo inategemea na msaada atakaopata lakini vinginevyo asipopata msaada wa matibabu tena kwa haraka anaweza kukatwa miguu“.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Baba Diamond alisema amepitia changamoto za muda mrefu kwa kusumbuliwa na miguu hiyo bila kupata matibabu hivyo ilifika wakati alikata tamaa ya maisha kabisa.
Kwa kweli miguu hii imenisumbua kwa muda mrefu sana. Nimehangaika katika hospitali nyingi tu lakini kwa kweli nimeshindwa kujitibia kutokana na gharama kuwa kubwa”.
Baba Diamond alipoulizwa kama ameshamwambia mwanaye amsaidie, baba Diamond hakutaka kumzungumzia lakini akasema anaamini kama ni tatizo hilo, Diamond atakuwa analifahamu vizuri maana lina muda mrefu.
Siwezi kumzungumzia sana lakini kikubwa mimi kwa sasa namshukuru Mungu kanikutanisha na dada kutoka Uingereza anaitwa Zubeda Humphries ambaye amekuja na kuahidi kunisaidia ili niweze kutibiwa”.