Baba Diamond Atoa Neno Kuhusu Ndoa Ya Diamond na Tanasha
Baba mzazi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Mzee Abdul Juma maarufu kama Baba Diamond amefungukia Ndoa Ijayo kati ya Mwanaye Diamond na Mpenzi Wake Tanasha Donna.
Wiki chache zilizopita Diamond alitangaza rasmi kwenye mitandao ya kijamii dhamira yake ya kumuoa mrembo kutoka nchini Kenya, Tanasha Donna ‘Zahara Zaire’ ifikapo Februari mwakani na kufanya watu wengi kuwa na hamu ya kushuhudia harusi hiyo.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi, Baba Diamond amesema ingawa Mpaka sasa hajapewa taarifa kuhusu Ndoa ya mwanaye lakini anatamani siku ya Ndoa wamualike.
Sijaambiwa habari za ndoa ila nasikia tu watu mitaani wanazungumzia suala hilo, kikubwa naomba iwe ya heri Mungu afanikishe nitafurahi sana mwanangu akioa lakini namuomba sana asiache kunialika, asiponialika nitaona amenidharau sana, nitajisikia vibaya”.