Baada Ya Mahakama Kutupilia Mbali Kesi Ya Mobeto, Wakili Wake Afunguka
Kesi ya mwanadada Hamisa Mobeto na mzazi mwenzie Diamond Platinumz iliyopelewa mahakamani mwezi uliopita ikihusisha hati ya madai ya mwanadada huyo kwa mzazi mwenzie kuhusu matunzo ya mtoto huku mwanadada huyo akitaka kulipwa milion tazo kama matunzo kwa mtoto iliyotupiliwa mbali na kusemekana kuwa mshtaki wa kesi hiyo alikosea baadhi ya masharti ya ufunguzi wa kesi hiyo hivyo mahakama kuitupulia mbali .
Hata hivyo watu wengi walidhani kuwa baada ya mahakama kutupilia mbali kesi hiyo basi ndio itakuwa mwisho wa madai hayo kutoka kwa upande wa mashtaka lakini kitu cha ajabu ni kwamba baada ya kesi hiyo kutupiliwa mbali , wakili wa mwanandada Hamisa Mobeto amefunguka na kuongelea swala hilo ni kusema kuwa kesi hiyo bado iko palepale.
Hata hivyo hilo alibadilishi chochote kwa sababu kesi ya msingi iko palepale, na jana baada ya mahakama kufuta kesi hiyo tulibadilisha haraka na kurekebisha yale yote yaliyokosewa na kuifungua upya ikiwa na marekebisho hivyom kesi ya msingi bado iko palepale.
Akiongezea wakili huyo amesema kuwa hata hivyo baada ya process hizo wanachosubiri kwa sasa ni kupangiwa tarehe nyingine upya ili waweze kwenda tena kusikiliza kesi hiyo mahakamani,
kwaiyo kwa sasa tunachosubiri ni kupangwa kwa tarehe mpya ya kusikilizwa kwa kesi hiyo mahakani,
Akimtetea mteja wake wakili Walter alisema kuwa watu wengi wamekuwa wakilaumu kuhusu kiwango anachodai Hamisa Mobeto kwa baba wa mtoto wake lakini ukweli ni kwamba Hamisa anaweza kuwa sahihi kwa sababu ya vitu fulani fulani,lakini pia kesi kama hizi huwa ni za muda mfupi na makwazo kama haya utokea ili kupoteza muda.
kwa kawaidia haya mapingamizi huwa yanawekwa kwa ajili ya kupoteza muda tu lakini kesi za madai kama hizi huwa hazitakiwi kuchukua hata miezi sita.
Hamisa alifungua kesi hiyo zidi ya Diamond huku akidai kupewa hela ya matumizi ya mtoto wake aliezaa na msanii huyo kiasi cha shilingi milioni tano kwa mwezi, hii ni baada ya msanii huyo kuonga kwenye media kuwa amekuwa akimuuhudumia mtoto huyo huku mwanadada huyo akikanusha usemi huo