Baada ya Lulu Diva Kujitapa Kununua Jumba la Milioni 100, Inasemekana Kuna Mkono Wa Waziri Umehusika

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayeendelea kufanya vizuri hivi sasa na ngoma yake ya ‘Mazoea’ ambaye siku chache zilizopita alijitapa kumiliki mjengo wenye thamani ya milioni 100 ambao alidai alinunua mwenyewe lakini kuna habari mpya zinazosema vinginevyo.

Siku chache zilizopita Lulu Diva aliuanika wazi mjengo wake mpya kwenye magazeti ya Global Publishers ambapo aliionyesha dunia nzima nyumba yake anayoishi kwa hivi sasa na pia gari lake la kifahari aina ya ‘Jeep’ analoendesha kwa hivi sasa.

download latest music    

Kwenye interview aliyoofanya na Millard Ayo Tv siku chache zilizopita Lulu Diva alifunguka haya kuhusu mjengo wake huo mpya:

Hivi vitu vyangu vyote nilivyonavyo nimenunua kwa kazi zangu za kimuziki lakini pia kuna kazi zangu nyingine nafanya kama biashara na kilimo na ile nyumba mliyoiona kwenye mitandao ya kijamii ikitrend ni yangu mwenyewe wala sijapangisha bali nimenunua ina vyumba viwili ipo maeneo ya Mbezi Beach nilinunua around milioni mia yaani haipungui milioni mia na kitu”.

Lakini sasa Global Tv online wanaripoti kuwa nyuma ya pazia kuna kigogo mmoja wa serikali ambaye jina kapuni ambaye amesimamia shoo nzima kuanzia kununua mjengo ule mpaka kuimalizia kuujenga lakini pia kigogo huyo pia amesimamia shoo ya gari analoendesha mrembo huyo kwa sasa.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.