Baada ya Kumjohi Diamond, TCRA Kuichunguza Times Fm
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA imesema kuwa kamati yake ya maudhui inafatilia kipindi alichofanya Diamond Platinumz katika radio ya Times Fm iliyofanyika siku za hivi karibuni huku kipindi hicho kikiongozwa na Lilommy.
Mkuu wa idara ya mamlaka hiyo amesema kuwa wameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuona mahojiano hayo na pia kituo icho kipo katika vituo wanavyovisismamia.
Diamond alifanya mahojiano na kituo icho na kusema mambo mengi ambayo hayakuwahi kujulikana katika jamii, lakini kubwa zaidi ni kufunguka hasira zake baada ya kufungiwa kwake na wasanii wenzake kupigwa kwa baadhi ya nyimbo zao katika vituo mbalimbali .
Kwa namna nyingine inaweza kusemekana kuwa mahojiano hayo ndio yaliyozua migogoro yote inayoendelea sasa kati ya Diamond na mamlaka ya inayohusiaka na mambo ya sanaa.