Baada ya Kubadili Dini, Charz Baba Afunga ndoa
Msanii wa miondoko ya dansi nchini , Charz Baba ameamua kukamilisha torati baada ya kuamua kufunga ndoa na mpezi wake aliemfanya abadilishe dini.
Hivi karibuni tetesi hizo ziliibuka kuwa mwanaume huyo ameamua kuadili dini huku lengo kubwa ikiwa ni kutaka kuoa mwanamke zaidi ya mmoja kitu ambacho alikanusha na kusema kuwa sio kweli ila amekuwa na sababu zake tofauti.
Wikiend hii msanii huyo aliamua kukamilisha torati yake ni baada ya kuamua kufunga ndoa hiyo na mwanamke wake ambae inasemekana kuwa ndio sababu kubwa ya yeye kubadili dini.