Baada Ya Jaji Kutoa Hukumu,Kumbe Lulu Alikataza Watu Kukata Rufaa
Ni dhahiri kuwa baada ya hukumu ya Lulu kutolewa na jaji wengi waliumia sana hasa kuondokewa na ndugu, rariki na mwanafamilia wa tasnia ya filamu Tanzania tena ikiwa nyota yake inaanza kungaa kwa style ya ajabu.Wakili Msomi na mtetezi wake aliyekuwa nae kwa kipindi chote cha kesi Bw. Peter Kibatala na alisimama mbele za watu na kuwatia moyo kuwa inawezekana kabisa Lulu kutoka kwa dhamana huku akiendelea kukata rufaa ya kutokurizika na hukumu hiyo.
Lakini kumbe faraja ambayo ilikuwa mioyoni mws watu inaweza kuanza kuyeyuka hasa baada ya kusikia taarifa kwamba tangu siku ya kwanza baada ya hukumu mwanadada mwenyewe Elizabeth Lulu Michael alikataa kata kaat ndugu zake wasifanye jambo lolote linalohusiana na kukata rufaa ya hukumu hiyo kwa sababu anataka kuheshimu maamuzi ya mahakama na kutumikia adhabu yake lakini pia alitaka kutumikia kifungoi hicho alichopewa na mahakama ili anapotoka huko awe huru na jamii inayomzunguka.
Akisimulia mambo yote yaliyotokea siku ya tukio, baba mlezi wa Lulu ambae alikuwa nae bega kwa bega katika kipindi chote hicho na ndie aliyemkuza katika tasnia ya filamu Dr.Cheni alisema kuwa
kwakweli Lulu ni kama alijua lolote linaweza kutokea siku ile,ingwa ilo la kufungwa hakulipa kipaumbele sana.jaji alipomaliza kusoma hukumu lulu alishtuka kama sisi lakini yeye aliekuwa wa kwanza kurudi katika hali yake ya kawaida na akaanza kutoa kauli za ujasiri. -Alisimulia dr.Dheni
sipingani na maamuzi ya mungu na haya ni maamuzi yake kabisa, na ana makusudi yake kunipa hiki kilichotokea leo,acheni miaka miwili ipite sio mingi sitaki kupingana na maamuzi ya mahakama.nayaheshimu sana maamuzi ya mahakama acheni nikatumikie kifungo changu.– Aliongea Dr.Cheni akiwa anarudia maneno aliyosema Lulu mahakamani siku ya mwisho ya hukumu yake.
hivyo basi kwa namna moja ama nyingne hata kama hakujua ilo litatokea lakini hakuwa mtu wa kuonyesha kukata tamaa kwa kile kilichomkuta siku ile.Elizabeth Lulu Michael anawekwa katika orodha ya wasichana wadogo Tanzania waliowahi kupata mafanikio kwa kupitia misukosuko mingi alkini bado hakuwahi kuteteleka.