Baada Ya Hukumu ya Lulu Kutolewa , Mama Kanumba Amwaga Chozi
Ikiwa ni dakika chache tu baada ya hukumu kutolewa leo Novemba 13 juu ya kesi iliyokuwa ikimkabili mwanadada Lulu Michael kuhusu kuua bila kukusudia ambapo msanii huyo amehukumiwa miaka miwili jela kwa kukutwa na hatia hiyo.
Mama wa marehemu Steven Kanumba ambae ndie alikuwa mpenzi wa eElizabeth Lulu Michael ameonekana nje ya mahakanma akilia kwa sauti hukua akisema kuwa anaishujkuru sana mahakama na serikali yake wa ujumla juu ya maamuzi waliotoa kuhusu kesi hiyo,mama huyo huku akilia amesema kuwa akitoka mahakamani hapo ataelekea makaburini alipolazwa Kanumba ili kwenda kumpumzisha kwa amani sasa tangu alipokuwa amezikwa .
mimi sina la kusem kwa sasa hivi ila la kwanza namshukuru mwenyezi mungu sana,pili ninaishukuru mahakama kwa kutenda haki na pia naishukuru sana seriakli yangu na hata nikitoka hapa nitaenda makaburini naamini sasa naenda kumzika na akapumzike kwa amani.-aliongea Mama Kanumba huku akilia kwa sauti
Kesi ya Lulu ambayo ilisikilizwa ushahidi wote mwezi uliopita ilikuwa imebaki kusikilizwa hukumu tu ambapo leo ndio ilikuwa mwisho wa kesi hiyo , hata hivyo leo tangu kumekucha kume kuwa na tension kubwa ya watu mbalimbali katika mitandao ya kijamii wakimuombea mwandada huyo kheri katika hukumu yake huku wengne wakiomba hasihukumuiwe kwa chochote,
Hata baada ya kutolewa wa hukumu hiyo watu wengi wameonyeshwa kuumizwa na hukumu iyo akiwepo Wema Sepetu ambao kwake ilikuwa ni habari mbaya tena ya kushtukiza sana.lulu atatumikia kifungio hicho cha kuua bila kukusudua kwa muda wa miaka miwili gerezani.
Lulu alikutwa na kesi hiyo mwaka 2012, ambapo alimuua Kanumba aliyekuwa mpenzi wake bila kukusudia kutokana na ugomvi wa mapenzi waliokuwa nao wawili hao ambapo katika purukushani hizo Kanumba alidondoakana kuanguka chini na ndipo mauti yalipomkuta.Hata hivyo baada ya kusikilizwa kwa ushaihidi kutoka kwa watu wa pande zote mbili mahakama imeamuru lulu kutumikia kifungo hicho baada ya kuona kuwa katika ushahidi wake mwandada huyo alishindwa kuongea vitu vyote vilivyokuwa vimetokea siku ya tukio.