Aunty Ezekiel Atamba Kuwa Hodari Wa Mapenzi
Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Aunty Ezekiel amefunguka na kujitambia kuwa yeye ni hodari wa mapenzi na kujisifia kuwa anapokuwa na mwanaume basi anafanikiwa kabisa kumtuliza na kuwa wake peke yake.
Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Risasi Jumamosi, Aunty alisema kuwa linapokuja suala la kumpenda mtu hata akiwa na nani atamuachia tu kwani anajijua ni hodari wa kuondoa wote waliokuwa kwenye himaya hiyo.
Siwezi kuanika moja kwa moja ninafanya nini na kwa nini wakiwa kwangu hawafurukuti, lakini najua wazi kuwa nina sifa hiyo na sijawahi kushindwa kwenye hilo”.
Hivi sasa Aunty yupo kwenye mahusiano na Baba watoto wake dancer Mose Iyobo ambaye ameshawahi kukiri kuwa siku za nyuma wakati wanaanza mahusiano alikuwa na wanawake kadhaa lakini tangu yuko naye ametulia na yeye peke yake.