Aunty Ezekiel Ataja Sababu Ya Kutoenda Kwenye Sherehe Ya Wema

Muigizaji wa Bongo movie Aunty Ezekiel ameweka wazi sababu ya kutoonekana Kwenye Birthday party ya rafiki yake kipenzi Wema Sepetu iliyofanyika siku chache zilizopita.

Siku ya Jumapili kulikuwa kuna bonge la party ya Birthday ya Wema Sepetu ambayo ilihudhuriwa na mastaa kibao lakini kati ya watu hao mtu ambaye alikosekana ni rafiki kipenzi wa Wema ambaye ni Aunty Ezekiel.

download latest music    

Aunty kutohudhuria kulizua maneno mengi ikiwemo watu kufikiri labda wawili hao hawana maelewano.

Kwenye mahojiano yake na waandishi wa habari Katika usiku wa Jibebe Challenge, Aunty amefunguka na kusema sababu iliyomfanya asihudhurie ni kukosa nguo ya kuvaa.

Kilichotokea ni kwamba kila kitu ambacho kilifanyika tulishirikiana kuanzia mwanzo hadi mwisho yaani kuanzia kutoa kadi mpaka mwisho Lakini pia mwishoni fundi akaharibu nguo yangu ikabidi nilale nyumbani hamna kingine”.

Aunty Ezekiel amekana tetesi za kuwa hajahudhuria sherehw ya Wema kwa sababu amemlipizia kwa sababu kama utakumbuka siku za nyuma Kwenye uzinduzi wa movie ya Aunty ya ‘Mama’ Wema naye hakuhudhuria uzinduzi huo Mlimani City akasema nguo yake iliharibiwa na fundi.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.