Aunty Ezekiel Ashangazwa Na Wanaohoji Urafiki Wake na Shamsa

Msanii wa kike ambae pia ni mjasiriamali bongo Aunty Ezekiel au Mama Cookie ameshangazwa na baadhi ya watu katika mitandao ambao wamekuwa wakitokwa na maneno lukuki baada ya kumuona yeye akiwa karibu na msanii mwenzie wa kike Shamsa Ford kama marafiki kwa kipindi cha hivi karibuni.

Wasanii hao wa kike ambao hawakuwa karibu sana hapo awali na hata kuwa marafiki kama walivyo saa wamekuwa wakionekana wakiwa karibuni kwa hivi siku za karibuni na kuwafanya watu kuwa na maswali kuwa urafiki wao umeanzia wapi gafla gafla kwa sababu hawajawahi kuwa marafiki wala hawaendani na hawafai kuwa marafiki wa karibu.

download latest music    

Hata hivyo kwa nyakati tofauti wasanii hao wa kike waliulizwa na hata wao walionekana kushangazwa na mashabiki wao kwa kitendo cha kuwa wanawachagulia marafiki wakati wao wote ni wanawake na wanafanya kazi katika tasnia moja, hata hivyo kwa upande wa Aunty Ezekiel alisema kuwa mashabiki wao wamekuwa wanakosa maneno ya kuongea  na kujikuta wanahoji kila kitu.kwa upande wake yeye anasema kuwa alishawahi kuwa na marafiki wengi kwa nini watu wahoji urafiki wake na shamsa.

Nimeshakuwa na marafiki  wengi sana kwanini wamekuwa wakihoji na kuongelea urafiki wangu na Shamsa. Alihoji Aunty Ezekiel.

Hii inaweza kuwa ni kwa sababu wasanii wengi sana wa kike wamekuwa na marafiki na kushindwa kudumisha uhusiano wa urafiki wao na hata wanapogombana wanaishia kutukanana katika mitandao ya kijamii.

 

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.