Aunty Ezekiel Afungukia Tattoo Yake Ya Paja
Muigizaji wa Bongo movie Aunty Ezekiel amefunguka na kumwaga povu zito kutokana na maswali ambayo amekuwa akipata baada ya kuanika tattoo yake mpya ya paja.
Siku chache zilizopita Aunty alivaa nguo fupi na Kujiweka kwenye Mitandao ya kijamii na kwenye paja lake la mguu wa Kulia alionekana akiwa na tattoo kubwa iliyozua maswali.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti La Ijumaa, Aunty alisema kwanza hiyo tatuu siyo halisi ameichora kwa piko ila watu wanavyomjadili amewezaji kufunua paja kuchora na wakati kuna watu wanaochora sehemu tofauti na za kushangaza.
Nawashangaa sana wanaojadili paja langu sijui wanachotaka ni kitu gani, kwanza hapa nimejichora tu na piko lakini kingine wameona kujichora hivi kama kitu kisicho cha kawaida inashangaza kwa kweli waniache na maisha yangu“.