Athari Za Mapenzi Mahala Pa Kazi
Endapo wewe unakuwa ni mfanyakazi basi sehemu kubwa ya maisha yako baada ya kuajiriwa itakuwa ni eneo lako la kazi, muda mwingi utakuwa ukikaa na wale wanaokuzunguka zaidi ofisini kuliko nyumbani.Kuna baadhi hata ya tabia zinaweza kuwa zinajulikana sana na wafanyakazi nwenzako kuliko hata familia yako, kitendo cha kuwa na muda mwingine na wafanyakazi wenzako kinaweza kukufanya uingie kwenye mtego wa kuanzisha mahusiano ya kimapenzi kazini ikiwa tayari ulishaoa au kuolewa au ndio unataka kuingia katika mahusiano.
Kwa kawaida kufanya kazi na mtu katika mazingira yaleyale ndio usababisha watu kupendana sana,wengi usema kuwa mapenzi katika mazingira ya kazi hayaepukiki,hii ni kweli kabisa kwa sababu muda mwingi mnakuwa pamoja.
Chukulia mfano unaondoka nyumban asubuhi sana na unarudi jioni sana, je utapata wapi muda wa kuonana na watu maeneo mengine, ukweli unakuja kwamba kumbe kazini ni moja ya sehemu inayoweza kukupa mpenzi wa kudumu.Lakini jitahidi kuwaza yafuatayo ukiwa unataka kuanzisha mahusiano hayo:
Ukaribu wenu unaweza kuwatenganisha na wengine
Ni vigumu kuficha hisia za mapenzi mbele za watu, mtajitahidi kuwa kimya ila kuna kipindi waliopo pembeni yenu wataanza kujua mahusiano yenu tu, na hapo ndipo zitaanza kutokea nyufa za matengano,kama mmoja wenu alifanya hivyo ili kupata mchepuko atakae mpa amani anapotoka katika mafarakano ya nyumbani basi mtaogopa habari kufikia mlengwa mmoja wapo, lakini pia mtakapokuwa mnasemwa ofisini mtahisi kama wenzenu wanawaonea wivu.
wapo watakaokuwa wanaheshimu hisia zenu na hata kuwa wanawapisha muwe na faragha na maongezi yenu, lakini kwenu inaweza kuwa ngumu kuelewa hivyo zaidi ya kuona kama manatengwa tu.
Mgongano wa kimaslahi.
Mapenzi yanaweza kuwa kikwazo katika utendaji kazi,ikiwa mmoja ni muajibikaji kwa mwingine na tayari mmeshaingiza swala la mapenzi katikati yenu itakuwa vigumu kutiliana mkazo au kuwajibishana kwa sababu tayari kuna mapenzi kati yenu.hali hii inaweza kukufanya ukawa mtoro, kuchukia kazi au kutokufanya kazi kwa umakini ukijua kuwa kuna mtu anaekukingia kifua eneo lako la kazi.
Ikitokea mkaachana.
Sio kila mahusiano yanadumu kama tunavyokuwa tunategemea pindi tunapoyaanzisha, hapana lakini ikitokea sasa mmeachana ni vigumu kuendelea kukaa sehemu moja na mtu ambae amekuwa akikujua kwa zaidi ya sana na bado mmegombana alafu mnakuwa mnapishana milangoni au kumtumiakia kwa kuwa inakubidi ufanye hivyo.
Upelekea kupoteza kazi.
Ikitokea mmeshagombana na mmekuwa maadui ni vigumu tena kuwa katika eneo moja hii itafanya mmoja wapo ambae hayupo huru kuondoka kutafuta amani yake,lakini pia endapo ikigundulika kuwa chanzo cha kutokuwa na ufanisi wa kazi kwa watu fulani ofisi unasababishwa na uhusiano wa kimapenzi uliojengeka baina yao basi ni rahisi mmoja kupoteza kazi au wote.