Aslay ampaka tope Saidi Fella

Mkurugenzi wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Saidi Fella maarufu pia kama Mkubwa Fella amekosolewa hadharani na msanii Aslay.

Akiongea katika kipindi cha Zero Planet cha Ice Fm, Aslay alisema kuwa Mkubwa hamsaidii msanii anayefanya kazi yake binafsi.

download latest music    

“Ni kweli Mkubwa yeye anasimamia Yamoto Band, Mkubwa hasimamii msanii mmoja mmoja, kwahiyo unatakiwa ufanye kitu cha ziada ilimradi ngoma zako zifike. Wenzangu wanaandaa vitu vinakuja lakini mimi nimefanya kama nimewahi kuwaonesha njia,”Aslay alisema.

Aliyosema Aslay yanapinga maneno Mkubwa Fella alisema hapo nyuma kuhusu kusupport wasanii wa Yamoto Bend wanaofanya miradi zao za kibinafsi.

Soma pia: Mkubwa Fella: Hakuna msanii aliyekatazwa kuondoka ndani ya kundi ya Yamoto Band

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere