Askofu Gwajima aachiliwa huru na Mahakama
Askofu Gwajima sasa hivi yuko huru baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumuachia baada ya upande wa mashitaka ushadi kukosa ushahidi wa kutosha baada ya kupelekwa kotini na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinari Pengo.
Kulingana na malalamishi ya Askofu Mwadhama inasemekana kuwa Gwajima alitumia lugha chafu na kuharibu jina la Mwadhama. Hata hivyo kesi hii imetupiliwa mbali baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuleta mashidi kwa muda wa miezi 14.
Hata hivyo wakili wa Serikali, Joseph Maugo aliomba mahakama kuhairisha kesi hiyo ili kuwapa muda tosha wa kupata mashahidi katika kesi badala ya kesi hiyo kufutwa.
Gwajima anasemekana kuwa aliluita Askofu Mwadhama Polycarp ; Ni mpuuzi mmoja mjinga mmoja asiyefaa mmoja anaitwa Askofu Pengo aliropoka sijui amekula nini mimi naitwa Gwajima namwita mpuuzi yule mjinga yule na kuonesha Pengo ni mtoto mpuuzi na mwenye akili ndogo na kwamba maneno hayo yangeweza kuleta uvunjifu wa amani