Amini Awataka Wasanii Wakongwe Kufanya Muziki Unaokwenda na Wakati
Mwanamuziki wa Bongo fleva aliyefanya vyema kipindi cha nyuma Amini amewachana wasanii wakongwe kuwa wafanye muziki ambao unaendana na mabadiliko ya wakati.
Kwa muda mrefu kumekuwa na kilio cha wasanii wakongwe kwa kushindwa kurudi Kwenye gemu jipya na kufanya vyema walivyokuwa wanafanya miaka ya nyuma.
Kwenye mahojiano na Bongo 5, Amini amewataka wasanii wakongwe kufanya kazi ambazo zitakuwa na sababu ya kupigwa kwenye vituo mbalimbali vya redio na runinga ili washindane na wasanii wapya.
Wasanii wengi wakongwe wamekuwa wakibusiana vichwa jinsi ya kurudi kwenye chati kwa hivi sasa kwani kuna wasanii wengi wapya wanafanya vizuri sana na ni ngumu kuwachomoa.
Tatizo kubwa wasanii wakongwe wanang’ang’ania kufanya mziki aliotoa mwaka 2003 wakati huu ni mwaka 2018 mambo yamebadilika na hata tungo zimebadilika na muda hivyo ni muhimu kwa wasanii hao kusoma mazingira kabla ya kukurupuka na kutoa nyimbo.