Amber rutty , Mpenzi Wake Kuamua Kuokoka.
Mchungaji, Daudi Mashimo amesema kuwa msanii Rutyfiya Abubakary maarufu kama ‘Amber Rutty’ na mpenzi wake Said Bakary baada ya kumdhamini msanii huyo yeye na mpenzi wake wamekubali kuishi maisha ya kumpendeza Mungu.
Mchungaji Mashimo akizungumza EATV, amesema kuwa Amber Rutty na mpenzi wake wameamua kabisa kufanya hivyo kutokana na yale waliyoyapitia lakini pia wamegundua kuwa maisha yao ya hapo awal hayakuwa ya mupnendeza mungu hata kidogo, alizungumzia swala hilo kwaajili ya maisha yajayo ya wasanii ha mchungaji anasema;-
“Kama mimi mchungaji mtumishi wa Mungu nimezungumza nao mambo mengi kwaajili ya maisha yajayo na hali iliyokuwepo ni watu ambao kweli kweli ni watu ambao mioyo yao imekunjuka na kufunguka na ni watu ambao wamekubali kuishi maisha ya kumpendeza Mungu,”alisema Mchungaji Mashimo.
Novemba 2, 2018 walifikishwa Mahakamani kwa kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile , kesi ambayo walikosa kabisa watu wa kuwadhamini na ndipo mchungaji huyo ambae alisema kuwa yeye ametumwa na Mungu atafanya kazi hiyo kama alivyoagizwa kiimani.