Amber Lulu Akiri Kutamani Mtoto Lakini Hali Ya Kiuchumi Inamzuia
Video vixen na msanii wa Bongo fleva Amber Lulu ameibuka na kuweka wazi kuwa anatamani sana kuzaa Mtoto Wake mwenyewe lakini hali kiuchumi ineluctable kikwazo kwake.
Amber Lulu amekiri kuwa anatamani sana kuitwa mama Kama ilivyo kuwa kwa marafiki zake wengine na hata wasanii wenzake lakini hawezi kwa sababu anaona kabisa kuwa ramani hazisomeki.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Amber alisema kuwa iwapo atapata mwanaume wa kuishi naye ambaye hana longolongo, ataanzisha naye familia lakini kwa sasa maisha yake ya kimapenzi hayaelewielewi.
Siyo kwamba sipendi watoto jamani lakini naona bado ramani haijasomeka kabisa maana siyo nazaa halafu hata ‘pampers’ ya kumvalisha mtoto nakosa, kitu hicho sikipendi kabisa, bado naangalia kwanza, kwani kuzaa sio fasheni”.
“