Amber Lulu Akiri Kubadilishwa na Penzi La Prezzo
Video queen na Msanii wa Bongo fleva Lulu Eugene maarufukwa jina la usanii Kama Amber Lulu ameibuka na kudai Mpenzi Wake Msanii kutoka Kenya Prezzo amembadilisha tabia yake.
Amber Lulu alianza mahusiano ya kimapenzi na Jackson Makini ‘Prezzo’ mapema mwaka jana Baada ya kuachana na Mpenzi Wake wa siku nyingi Young Dee lakini wawili hao waliachana kwa miezi michache lakini sasa wapo pamoja tena.
Katika mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda,Amber Lulu alidai kuwa Prezzo alishindwa tabia zake akaamua kukaa pembeni lakini kwa sasa amebadilika sana ndiyo maana wameweza kuwa pamoja tena.
Baada ya kubaini ugomvi wetu chanzo kikubwa kilikuwa ni tabia yangu niliamua kubadilika, nikaacha yale ambayo mwenzangu alikuwa hayapendi ndiyo maana hata kwenye mtandao wa Instagram nimebadili hata vitu ninavyotupia tofauti na zamani nilikuwa natupia picha za aibu”.