Ally Nipishe Akumbwa Na Tuhuma Za Kutelekeza Mtoto

Imekuwa  kama tabia na sifa zilizojengeka kwa baadhi ya wasanii  wa kiume kukataa watoto wao , kwa Tanzania idadi ya  wasanii wenye tabia hii  inazidi kuongezeka siku hadi hadi siku.Huku shida ya malezi inabaki kuwa kwa mama wazazi wa watoto hao, na wasanii wengine wakiwatuhumu wazazi wa kike kuwa walikuwa wakibambiza mimba hizo.

Msanii wa Bongo  Ally Nipishe ameingia katika headline za baaadhi ya vyombo vya habari baada ya kutuhumiwa kutelekeza mtoto aliyezaa na mwanamke ambae wameshaachana kwa sasa.Msanii huyo  alisikika katika kipindi cha Tv cha Family Love  kinachoonyeshwa na clouds tv kikiongozwa na Gabo alisema kuwa anamtoto mmoja na yeye ni baba mzuri katika malezi ya mtoto huyo na amekuwa akimuhudumia mahitaji yote ingawa hana mahusiano mazuri na mama mzazi.

download latest music    

Lakini hali imekuwa tofauti babada ya mama mzazi wa mtoto huyo kuibuka na kusema kuwa sio kweli kuwa msanii huyo anachosema kuhusu kutoa matumizi na mahitaji kwa mwanae kwa sababbu amekuwa hamuudumii mtoto wake.Huku baadhi ya ujumbe wa sms aliouonyesha  kuhusu mawasiliano ya wazazi hao wawili unaonyesha  Ally Nipishe alivyomwandikia mama huyo na kumwambia kuwa yeye hawezi kujidhalilisha katika vyombo vya habari kuhusu malezi ya mwanae kwa sababu yeye ni msanii, hivyo msanii huyo aliogopa kukiri kuwa hatoi matumizi kwa mtoto wake kwa sababu alijua hiyo ni moja ya aibu zitakazimpata na zinaweza kushusha jina lake katika sanaa.

Hata hivyo katika mengi aliyozungumza mzazi mwenzie na Ally anasema kuwa yeye aliachana na Ally Nipishe baada ya kushindwana tabia na msanii huyo ambae alikuwa anaonyesha drama nyingi,  akama kurudi usiku sana au kutorudid nyumban kabisa hata wiki nzima ilhali walikuwa wote wanakaa nyumbani kwa mzazi wa mwanamke.

Vita kati wa wazazi hao inazidi kupamba moto kwa sababu kila mmoja anaonekana anavutia upande wake, akiongea katika eNews ya EATV Ally Nipishe alisema “Mama Fetty anaishi na bwana wake, Fetty anaishi na bibi yake hivyo mimi siwezi kumtumia ela mama yake , ntamtumia yule anaemlea mwanangu”

Wakati huohuo Mama Fetty nae alisema “maswala ya mimi kuishi na bwana wangu yeye hayamuhusu, tulishaachana na tulishaacha kusaidiana miaka mingi,yeye  amtumie ela yule anaelea mtoto, kama anatuma hawaonyeshe miamala” alifunguka Mama Fetty.

Hata hivyo Ally Nipishe katika kujietea kwaka anasema kuwa Mama Fetty  anaonekana bado anampenda na anataka waishi pamoja lakini yeye kwa sasa hayupo tayari.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.