Aliyezaa na Agness Akiri Kumkataza Marehemu Kumuanika Mtoto Mitandaoni
Baba mzazi wa Sania, ambae ni mtoto wa marehemu Agness Masogange amefunguka na kukiri kuwa ni kweli walikuwa wakimuzuia Agness kumuweka na kumuanika mtoto wao katika mitandao ya kijamii kwa sababu kila mtoto anakuwa na ndoto zake za baadae na sio kitu kizuri kwa sababu yule bado ni mtoto.
Mwanaume huyo alisema kuwa pamoja na kwamba yeye na aAgnes walikuwa hawaishi pamoja kwa muda mrefu tangu walipobahatika kupata mtoto lakini agness alikuwa ni zaidi ya mzazi mwenzie kwake kwa sababu walikuwa wkisaidia katika malezi ya mtoto wao.
Baba Saniaa anaelezea kuwa mwaka 2002/2003 walibahatika kupata mtoto na walikuwa wakikaa pamoja lakini alikuja akapata safari ya kwenda nje ambapo alidumu na kukaa huku kwa takribani miaka miwili na nusu hivyo alijikuta akianzisha uhusianao na mtu mwingine huko nje ya nchi na ndipo aliporudi Tanzania alimkuta Agness pia akiwa na mwanaume mwingie lakini kipindi hicho mtoto wao alikuwa akiishi kwa dada yake ambae ni shangazi yake Sania.
Hata hivyo baba sania anasema kuwa kitendo cha mtoto wao kusihi kwa shangazi yao waliafikiana baada ya kuona kuwa wote walikuwa bado wadogo na ilikuwa ni vigumu kumuachia agness kulea mtoto peke yake hivyoaliona bora akaake kwa shangazi yake.
Akielezea kiundani zaidi, baba sania anasema kuwa Agness alikuwa rafii yak sana pamoja na kwamba walikuwa wameachana lakini hawakuwahi kuwa maadui kwa sababu wakikuwa wana lengo la kumlea mtoto wao katika misngi mizuri na hivyo kuondokewa na agness ni pigo kubwa sana kwake.
Akizungumzia swala la maendeleo yamtoto hasa katika kipindi hiki ambacho mtoto amempoteza mama yake, baba yake Sania anasema kuwa mtoto wao amekuwa mpweke sana kuna muda anakuwa anakosa raha kabisa hivyo wanakuwa na jukumu la kuwa nae karibu ili kumuondolea hiyo hali.
Kwa kumalizia mzazi mwenzie na marehemu Agnes anahaidi kuwa njia pekee aliyoichagua ya kumuenzi na kumkubuka Agness ni kwa kumlea vizuri binti yao na kuhakikisha anapata kila kitu ambacho marehemu alitaka mtoto wake akipata na kutimiza ndoto zake.