Alikiba Aongea Kuhusu Mange Kimambi
Msanii wa Bongo anaefanya vizuri na kibao chake cha ‘seduce me’, Alikiba amefunguka na kuongelea mahusianao yake na mwanadada mtanzania anaishi Marekani anaejulikana kama Mange kimambi,mwanadada huyo ambae siku za nyuma baada ya kutoka kwa wimbo wa seduce me alionekana kuusifia sana wimbo huo na anaonekana ni mmoja wa mashabiki wa Alikiba. Hata hivyo kuna baadhi wa mashabiki wamekuwa wakisema kuwa mwanadada huyo ni team Alikiba na anatumia fursa hiyo kuwaponda team pinzani na hiyo .
Kwa mara nyingi katika posti zake kwenye ukurasa wake wa instagram mwanadada Mange Kimabi amekuwa akimpa sapoti msanii Alikiba tena hasa inapotikea baadhi ya watu wanaotaka kuonekana kumpondea msanii huyo.
Msanii huyo ambae kwa sasa anajizolea mashabiki wengi na amekuwa akifanya vizuri katika kazi zake amefunguka na kudai kuwa yeye na Mange ni mtu na shabiki yake na kwa babati nzuri alishawahi kukutana nae alipokuwa nje ya nchi kipindi cha nyuma na kupiga nae hadi picha akiwa kama shabiki wake na anafuraha sana pale ambapo idadi ya mashabikai zake inapozidi kuongezeka mapaka nje ya nchi ya nchi.
Akiongea na Bongo5, msanii Alikiba alisema kuwa ni ‘kama shabiki wangu na nimekuwa nikiappriciate sana , anapenda sana muziki wangu kwa sababu mimi ninamuheshimu kila mtu ambae kwa namna moja ama nyingine anani- sapoti katika kazi zangu lakini pia kutokana na uhuru kila mmoja ana haki, vilevile mimi nina haki ya kupendwa na mtu yeyote yule, hivyo nina haki ya kupendwa na Mange Kimambi pia” aliongea Alikiba
Hata hivyo anasema kuwa anakuwa furaha sana pale anapoona muziki wake unazidi kupanuka na kufika mbali kwa sababu unasikilizwa na watu maarufu, “nasikia furaha zaidi pale ninapoona watu wanaojulikana na maarufu nao wanafurahia muziki wangu si kusikia tu bali pia kuwa wao ni mashabiki wangu,, hivyo kwangu mimi ni raha sana , nawapenda sna mashabiki wangu wote duniani kwani nyinyi mnanipa furaha na amani” aliongezea Alikiba.