Alikiba Akumbwa na Tetesi za Kutelekeza Mtoto.
Ilikuwa imezoeleka kuwa Diamond ndio msanii amekuwa kila siku anakumbwa na tetesi za kutupa na kutelekeza watoto kwa mama zao, sasa wiki hii yamezuka makubwa baada ya ukurasa mmoja wa instagram unaosemekana kumjua Alikiba na mama wa mtoto wake kwa kuwa wote wanakaa mtaa moja kuwa msanii huyo ameacha kutoa matunzo ya mtoto wake wa kike aliyepo maeneo ya Ilala ambapo pia anakaa msanii huyo.
Katika page hiyo ambayo inaonekana kujua details nyingi za Alikiba anandika kuwa kwa muda mfupi alikuwa akiwasiliana na mama wa mtoto , Alikiba ameacha kutoa matunzo ya mtoto wake wa kike hivyo anaombwa kufanya hayo mapema kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa.
Mama mzazi wa mtoto huyo amesema kuwa mtoto wake kwa sasa anateseka kwa sababu ya kukosa matunzo na malezi ya wazazi wake wote wawili na hata kama hana mapenzi na mama wa mtoto basi anamuomba atoe tu matunzo kwa mwanae.
Alikiba najulikana kuwa ana watoto wawili wa kike na wa kiume lakini kumbe yupo mwingine ambae amekuwa hatoi huduma kwake wala kumuweka katika mitandao ya kijamii.
Hata hivyo inasemekana kuwa mzazi wa kike wa mtoto huyo ameamua kupeleka kesi hiyo katika vyombo vya dola ili kupata haki ya mtoto wake huyo hivyo siku yoyote bomu ilo litalipuka kuhusu msanii huyo kutelekeza mtoto.