Aliekuwa Mume Wa Irene Uwoya Afariki Dunia
Aliekuwa mume wa msanii wa bongo movie Irene Uwoya maaarufu kama Ndikumana afariki Dunia jana usiku.Ndikumana alikuwa maarufu kutokana na umahiri wake katika soka na mpaka mauti yanamkuta alikuwa akichezea timu ya APOP Kinyras Peyias ya nchini Cyprus.
Hamad Ndikumana alikuwa na umri wa miaka 39 kutoka nchini Rwanda alifariki usiku wa kuamkia leo ikisemekana kuwa alikuwa na matatizo ya moyo lakini alikuwa akiendelea na kazi zake kama kawaida.
Ndikumana na Irene Uwoya hawakuwahi kutengana kisheria lakini hawakuwa pamoja kwa takribani zaidi ya miaka mitatu nyuma lakini walikuwa wamebahatika kupta mtoto mmoja wa kiume.
Mpaka mauti yanamfika Ndikumana na Irene Uwoya walikuwa katika mafarakano na kutupiana maneno katika mtandao kutokana na irene uwoya kufunga ndoa na msanii mwenzie upande wa bongo fleva Dogo Janja .
Irene uwoya akiwa na Ndikumana siku ya harusi yao
Marehemu ndikumana akiwa na mtoto wake aliezaa na Irene Uwoya