Alichosema Profesa Jay Kuhusu Wasafi Tv
Kufunguliwa kwa kituo cha televisheni cha wasafi tv imekuwa moja ya stori kubwa mjini hasa baada ya kuona kuwa wasanii wengi wanaonekana kupata matumaini kuhusu kuwepo kwa kituo hicho kipya kama kauli mbiu yao inavyosema kuwa ni televisheni ya’ kwetu sote’
Diamond amepokea pongezi nyingi sana kutoka kwa wasanii na watu mbalimbali na pia moja ya wasanii wakubwa na wakongwe Profesa Jay hakuwepo nyuma kuzungumzia swala hilo pia.
hili ni jambo jema sana ambalo kwa kila mpenda maendeleo na burudani nchini ni lazima alifurahie,hongersa sana mdogo wangu @diamondpaltinumz na timu yako nzima ya WCB #YAMETIMIA TUKO PAMOJA SANA.- Aliandika profesa jay katika ukurasa wake wa Twitter.