Ali Kiba Ndiye Msanii Pekee Asiyehitaji Kiki Wala Matusi Kujaza Shoo-Mange Kimambi
Mwanaharakati wa mambo ya siasa mtandaoni Mwanamama Mange Kimambi ameibuka na kumpigia saluti staa wa Bongo fleva Ali Kiba na kudai kuwa hakuna Kama yeye Bongo nzima.
Mange ameongea hayo Baada ya shoo iliyofanyika Wiki iliyopita mjini Kahama kujaza nyomi la ajabu pamoja na kwamba Ali Kiba hakuipigia promo shoo Ile Kama ilivyokuwa kwa Wasafi Festival na Fiesta.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mange Kimambi ameandika maneno haya:
Ujumbe huo umeonekana Kama Dongo kwa mpinzani wa Ali Kiba Diamond Platnumz na tamasha lake la Wasafi Festival ambao walionekana kutoa promo ya nguvu Lakini pia Fiesta ambayo ilikuwa katika majobizano na Wasafi.