Ali Kiba Afungukia Tetesi Za Ujauzito Wa Mke Wake
Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Ali Kiba amefunguka na kuongelea tetesi zinazoendelea kusambaa kuwa mke wake wa Miezi Sita Amina Khaleef ni mjamzito.
Taarifa za ujauzito wa Amina zilianza kusambaa tangu walipofunga ndoa Miezi michache iliyopita lakini hijawahi kuthibitishwa kama ni kweli au uongo mpaka hivi sasa.
Kwenye mahojiano yake na kipindi cha Enews ya EATV, Ali Kiba ameweka wazi kuwa mke wake hana ujauzito ila huo ni ugumu tu uliotengenezwa Kwenye mitandao ya kijamii:
Kuna taarifa niliziona Kwenye mitandao ya kijamii kuwa mke wangu ni mjamzito lakini taarifa hizo sio za kweli, Kwenye ile picha iliyosambazwa mke wangu alikuwa amevaa koti langu ambalo lilitunishwa na upepo akaonekana kama mjamzito lakini hana mimba yupo sawa tu”.
Lakini pia Ali Kiba amesema watu hawamuoni mke wake akiwa naye kila wakati kwa sababu ni msomi ambaye anafanya kazi zake ambazo zibamuweka busy kila wakati na pia mkewe hapendi umaarufu na kujionyesha.