Ali Kiba Afunguka Baada Ya Kuburuzwa Mahakamani Kisa Kutelekeza Mtoto
Mwanamuziki wa Bongo fleva Ali Kiba anayefanya vizuri na ngoma yake mpya ya ‘Mvumo wa radi’ amefunguka na kujibu tuhuma za kutelekeza mtoto hadi kupelekea kufikishwa mahakamani.
Wiki iliyopita kuna habari ilitawala vyombo vya habari kuwa Ali Kiba amefikishwa mahakamani na mzazi mwenzake anayeitwa Khadija aliyezaa naye mtoto mmoja kwa kudaiwa Kutompa matunzo mtoto huyo.
Kwenye Interview na Kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, Kiba amedai mzazi mwenzake huyo aliinyanyasa sana familia yake kwa sababu alikuwa hataki kabisa mtoto aishi kwa upande wa wazazi wake.
Mtoto nilikuwa namlea vizuri tu, kila wikiendi alikuwa anakuja nyumbani na kama kumuhudumia natimiza majukumu yangu, sijajua sababu ya mwenzangu kuniletea fujo ila sijawahi kupelekwa Polisi.
Mimi niliiona kwenye gazeti, hayo malalamiko yapo Ustawi wa Jamii, haya yalitokana na mama yule alivyokuwa akitunyanyasa sisi sote familia yetu kuuhusu kukaa na mtoto ama kumuona.”.
Lakini pia Alikiba amesema amefurahi kuitwa mahakamani kwani haelewi mpaka sasa lengo la mzazi mwenzake huku akidai kuna kipindi mtoto anafikia hadi hatua anataja jina lingine la baba yake kitu ambacho kilimfanya aache kutoa huduma kwa mtoto.
Mimi nilikuwa nataka ifike huko ilipofika (Mahakamani), sababu haiwezekani kama kumuhudumia mimi nilikuwa namhudumia tena vizuri tu. Mtoto nimemtoa kwenye shule aliyokuwa akisoma, nikampeleka shule ya gharama zaidi ya mara tatu ya ile aliyokuwa akisoma mwanzo. Sasa yanapotokea haya nashindwa kuelewa lengo lake ni ini?”