Afande Sele Aipongeza Serikali kwa Kuwafungia Wasanii.
Msanii mkongwe wa muziki bongo ambae kwa sasa ameacha kufanya kazi za muziki Afande Sele leo amefunguka na kuipongeza serikali kwa hatua waliochukua ya kuwafungia wasanii ambao wanatoa nyimbo ambazo hazina maadili katika jamii.
Afande Sele alisema kuwa kuna wasanii ambao alikuwa akiwaona alijua kuwa watakuja katika tasnia kuendeleza muziki huu vizuri lakini kitu cha ajabu ni kwamba wamekuwa wa kwanza kuimba nyimbo za matusi na kuuharibu muziki kabisa.
Wasanii wa sasa hivi wanaimba sana mapenzi, ngono, kubakana,pombe ,ndoa kuvunjika, na mambo ya kunajisiana tu.
Nasikitika sana kuona kuwa wasanii ambao nilidhani watakuja katika tasnia kuwa warithi wetu kwenye vipaji vya hip- hop lakini wamebadilika leo ndio wanaimba matusi ya kijinga.
Pongezi za Afande Sele zimekuja baada ya serikali kupitia naibu waziri wa habari kuwafungia baadhi ya wasanii na nyimbo zao kutokuchezwa katika vituo mbalimbali vya habari kutokana na kutokesana kwa maadili .Hata hivyo baraza limesema kuwa halitaishia hapo katika kufungia wasanii wanaoimba vitu visivyo na maaadili badala yake wapo kwenye mhkato wa kuchunguza nyimbo zingine zenye mapungufu pia.