Abdul Kiba Akanusha Kuachana na Mkewe
Msanii kutoka katika kundi la Kings music amefunguka na kukanusha tetezi zinazosambaa juu yake kuwa ameachana na mke wake na kwamba ameamua kumrudisha nyumbani , na kwamba maisha ya ndoa yamemshinda.
Abdul Kiba amefunguka na kusema kuwa ni kweli kwa sasa amekuwa haishi na mke wake kwa sababu za kiafya , mke wake amekuwa akiumwa na kwamba anahitaji uangalizi wa karibu na ndio maana aliamua kumpeleka katika familia yake.
Abdul Kiba anasema kuwa yeye na mke wake hawajawahi kuachana, kugombana wala kupishana kauli kama vile watu wanavyosema katika mitandao ni umbea.
mimi na mke wangu hatujawahi kugombana wala kupishana, kwa kuwa sisi ni watu wazima na nimekuwa nikimpenda sana mke wangu siwezi kumuacha.
Habari z abdul kiba kuachana na mke wake zimekuwa za muda mrefu kidogo huku sababu kubwa ikisemwa kuwa ni mahusiano ya nyuma ya mwanamuziki huyo.