Wema Sepetu:Mohombi Ni Shemeji Yangu
Moja ya nyota wa kike katika tasnia ya filamu Tanzania, Wema Sepetu amefunguka na kueleza jinsi anavyokerwa na tabia za watu kuwa wanamzushia habari ambazo si za kweli tena hasa kwa sasa hivi karibumi kuwa ametoka kimapenzi na msanii mkubwa Duniani ambae alikuwepo hapa nchi wiki iliyopita.
Msanii huyo anaejulikana kwa jina la Mohombi alikuwepo nchini Tanzania wiki iliyopita katika uzinduzi wa album ya msanii wa kike Vannesa Mdee ambapo kuna baadhi ya nyimbo wameimba wote.Hata hivyo katika watu waliopata kuwa karibu na msanii Mohombi na kupiga nae picha ni Madame Wema Sepetu ambapo baada ya picha hizo kuonekana katika mitandao ya kijaimi ilianza kusambaa kuwa msanii huo mkubwa Duniani ametoka kimapenzi na Tanzanian sweetheart Wema Sepetu.
Akikanusha taarifa hizo Wema anasema kuwa kitendo cha kupiga picha na Mohombi ni kawaida kwa sababu ni shemeji yake na ana uhusiano na mtu wake wa karibu na ipo siku akiamua atamueka wazi mtu huyo.
hivi kwanini watu wanakuwa wepesi hvyo wa kuongea mambo,Mohombi ni shemeji yangu kama watu wanataka kumjua mpenzi wake ipo siku watamjua hivi karibuni tu, kwani nimepanga kumuanika waache kuotea otea.Alisema Wema Sepetu alipokuwa akijibu mbaadhi ya maswali alipokuwa akiongea na Bongo mix.
Wema amekuwa ni moja ya mastaa wa kike wachache ambao wanakumbwa sana na tuhguma za kujiingiza katika mapenzi na wasanii wengi wakubwa na kutokudumu nao katika mahusiano na tetesi za wema kuwa na baadhi ya watu maarufu kutoka nje wamekuwa wakimtumia kwa mara moja na kumuacha zimekuwa nyingi lakini hata hivyo yeye mwenyewe amekuwa akikana na kutafuta watu wanaomzushia taarifa hizo.