Sugu na Faiza Vitani Tena Safari Hii Kisa Nguo Ya Ndani (chup*)
Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ameingia tena kwenye vichwa vya habari baada ya kugombana tena na mzazi mwenzake muigizaji na mfanyabiashara Faiza Ally.
Hii sio mara ya kwanza kwa Faiza na Sugu kurushiana maneno maneno mtandaoni huku mara nyingi Faiza huanza kumrushia maneno Sugu na huishia kumtukana na kumkashifu maneno ya nguoni.
Mara nyingi Faiza anapenda kumtuhumu Sugu kuwa hatoi pesa ya matunzo ya mtoto wao wa kike waliyezaa wote Sasha na kufikia hadi hatua ya kusema kuwa Sugu pamoja na kuwa mbunge anashindwa kutoa pesa kwa ajili ya ada ya mtoto wake jambo ambalo Sugu analikataa mara kwa Mara.
Siku ya Jumapili Faiza kwa kupitia ukurasa wake wa Instagram aliwashangaza watu wengi baada ya kuanza kutoa historia ya nguo yake ya ndani (chupi) aliyokuwa anaivaa wakati ana uhusiano na Sugu ambapo Faiza alidai kuwa ilikuwa ngumu kwake kuacha kuivaa chupi hiyo kwa sababu ilimkumbusha mpenzi wake Sugu ambaye walikuwa wameachana kwa kipindi hicho alikuwa anavaa chupi hiyo iliyotoboka ili asimsahau.
Baada ya stori hiyo kusambaa kwenye mitandao ya kijamii Sugu alimjia juu Faiza na kumtolea povu ziti ambapo kupitia ukurasa wake wa Twitter Sugu aliandika kumtaka Fails waheshiamiane na aache mara mija utoto kwani alijua wazi kabisa kuwa ujumbe ule ulikuwa wake.