Jumbe Athibitisha Kufanya Mazungumzo na Rayvanny Kabla Ya ‘Siri’ Kutoka
Msanii mkongwe wa muziki wa lumba nchini Mzee Jumbe amefunguka na kukiri kuwa walishakutana na msanii Rayvanny kwa ajili ya kufanya mazungumzo nae kabla ya kutoa wimbo wake wa Siri ambao amrudia baadhi ya sehemu ya wimbo huo wa mzee huyo.
Mzee Jumbe amesema kuwa katika kurudia wimbo huo, Rayvanny na uongozi wake walimwita na kuongea nae vizuri na hata kumlipa kiasi cha pesa kizuri ambacho ameridhika nacho na kumruhusu kufanya wimbo huo kwa amani kabisa.
Akiongea kwa furaha na kuthibitisha hilo, Mzee Jumbe amesema kuwa amefurahi kuona Rayvanny ameutendea haki wimbo huo na anasema kuwa sababu kubwa ya kukubali Rayvanny kufanya wimbo huo ni kwa sababu anajua kuwa kundi la Wasafi na wasanii wake wanafanya kazi nzuri.
Wamenilipa vizuri na Rayvanny ameufanyia haki wimbo huo na nimekubali kwa sababu ninajua kazi nzuri sana wanayoifanya wasanii kutoka kundi la wasafi.
Mzee Jumbe ametoa shukrani zake za dhati kwa lebo ya wasafi na kusema kuwa anaona fahari kuona wamemkumbuka na kuukumbuka wimbo wake kwa sababu watu wengi wamekuwa wakiupa kisogo wimbo huo.
Ukitaka kuona hata katika video ya wimbo huo,nimetoka na huo ndio uungwana , mtu anatumia kazi yako na anakushirikisha mwenyewe na hata kama wasipokulipa unapata faraja.nashauri wasanii wengine wa kizazi kipya wafanye kazi na wasanii wakongwe ili wapate madini ya muziki na muziki wao utadumu , kama utakumbuka wimbo huu nimeuimba miaka mingi iliyopita lakini mpaka leo unafanya vizuri.
Mzee Jumbe ansema kuwa aliutoa wimbo wake mwaka 2001,na hata wimbo wa Rayvanny alishauri uitwe mapenzi ya siri lakini wakaona bora wauite siri.