Mastaa Wa Kike Wananitafuta Sana Tutengeneze Kiki
Mwanamuziki wa Bongo fleva Sam Wa Ukweli amefunguka na kudai kuwa ni kawaida yake kutafutwa na mastaa mbali mbali wa kike wakitaka wafanye matukio watafute kiki.
Sam Wa Ukweli amedai hayo baada ya kudai anarudi rasmi kwenye Bongo fleva baada ya kupumzika kwa kipindi kirefu. Sam alirudi kwenye vichwa vya habari baada ya Meneja aliyekuwa anasimamia kazi zake Meneja wake ‘Maneno’ kudai kuwa wakati wanafanya kazi wote Sam alikuwa anaenda sana kwa waganga ili muziki wake ufanye vizuri kauli ambayo Sam amedai pia ilikuwa yakutafuta kiki.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa TV Sam wa Ukweli alifunguka yafuatayo:
Wapo wanawake wanaonifuata mastaa wanataka wawe na mimi ili tutengeneze kiki lakini sasa na mimi nakuwa naangalia inanipa nini lakini nisingependa kuwataja hewani maana naweza nikagombana nao lakini wapo wengi wengine mastaa wa Bongo movie wamenifuata wanaaniambia wanataka kutoa movie lakini kuna kitu wanataka kufanya ili kiwe tofauti kwaiyo nauliza na mimi nitapata nini maana nisije nikachafuka tu wakati mimi nina familia yangu”.