Gigy Money:Hakuna Uhuru Tena
Msanii wa nyimbo za bongo fleva nchini Gigy Money ambae pia alianza kwa kujulikana katika tasnia ya sanaa kwa kuwa video vixen, jana aliitikia wito wa kuitwa na ofisi za BASATA baada ya kuingizwa kwenye list ya wasanii wa kike wanavaa vibaya na kutupia picha za uchi katika mitandao ya kijamii.Gigy Money ambae inasemekana kuwa alipigiwa simu na Naibu Waziri wa habari na michezo Mh. Juliana Shonza lakini hakujibu simu wala meseji jana aliamua kufika baada ya taarifa za kuitwa kwake kumfikia kupitia vyombo vya habari.
Hata hivyo mwanadada huyo baada ya kutoka katika ofisi za BASATA alionekana mwenye huzuni na kumwaga machozi kutokana na kile alichokutana nacho ndani ya ofisi hizo japokuwa hajasema moja kwa moja kuhusu nini ameambia kufanya kama adhabu au marekebisho makubwa ya kazi yake lakini bado amepewa maagizo ya kuonana na Naibu Waziri..
Akiendelea kuongea na waandishi wa habari Gigy Money alisema kuwa kwa sasa hakuna tena uhuru kama zama.”Mimi nitaongea na naibu waziri kama wanavyodai, lakini there is no freedom, hamna freedom tena, no freedom trust me mtu anakuja na ku-judge pia ya March.”
Lakini pia Gigy Money anasema kuwa BASATA wamemwamuru kujitambulisha na kujiandikisha kwa sababu amekuwa akifanya vitu bila kuwa na kibali cha kuwa msanii au video vexen kwa kipindi chake chote alichokuwa katika sanaa.
Akiendelea kuongea Gigy Money pia ametoa malalamiko yake na kusema kuwa amehangaika sana kulitengeneza jina laka e na kuna kipindi alikuwa mpaka akilia na kulalamika alipokuwa akilipwa ela ndogo chini ya kiwango cha kazi zake lakini hakuna aliyetokea kumsaidia kwanini sasa hivi watokee na kumhukumu tu.
Kwa kumalizia Gigy Money alisema kuwa kama haki yake ipo na basi itapatikana tu , lakini atafata kama walivyomtaka afanye na ataonana na naibu waziri ili kuitikia wito.
Gigy Money anaingia katika list ya wasichana watatu waliotajwa juzi na mh juliana shonza kuwa wanongoza kwa kuchapisha picha za uchi katika mitandao yao ya kijamii na kuwa wamekuwa mstari wa mbele kuvunja maadili, ambapo wenzie wawili ni msanii Pretty Kindy na Sanchi.