Mama Mobetto Afungukia Tuhuma za Kuchukuliwa Bwana na Mama Diamond
Mama mzazi wa mwanamitindo Hamisa Mobetto, Mama Mobetto amefunguka kuhusu tuhuma anazorushiwa kuwa amechukuliwa bwana na mama mzazi wa Diamond Platnumz, Bi. Sandrah.
Kipindi cha nyuma kabla Diamond na Hamisa hawajavurugana kuhusiana na kuzaa pamoja, Familia zao zilikuwa marafiki ikimaanisha hapo mwanzoni Mama Mobetto na Bi. Sandra walikuwa marafiki wazuri tu lakini baada ya sakata urafiki ulikata.
Mwaka Jana mwishoni Mama Diamond alitangaza kuwa ameolewa na mwanaume aliyejulikana kwa jina la Shamte jambo lililowashtua wengi kwa sababu hasa ya tofauti kubwa ya kiumri iliyoonekana lakini tangu kipindi hiko maneno Mengi yamesemwa kuhusiana na mume wa Bi. Sandra ambapo imesemekaa kuwa mara ya kwanza alikuwa ni bwana wa Mama Mobetto pakini shoga ake new kipindi hiko Bi. Sandrah alimuibia na kuolewa naye yeye.
Baada ya habari hizo kusambaa kwenye mitandao ya kijamii Mama Mobetto ameongea na Global Publishers na amekataa tuhuma hizo na kudai yeye na Shamtr ni walikuwa marafiki wazuri tu lakini sio vinginevyo:
Huyo kaka (Shamte) namjua kama rafiki yangu tu na kuwa na uhusiano wa kimapenzi hata mara mora moja. Nashangaa mno kuona watu wanakomalia Kama mimi nilikuwa nina uhusiano naye wa kimapenzi lakini siku zote watu wakiamua kusema nawaacha waseme au wafanye wanavyotaka wao”.