Mh.Shonza Aanza Na Gigy,Sanchi na Pretty Kindy
Ikiwa ni siku chache tangu Naibu Waziri wa habari Mh.Juliana Shonza kutamka kuwa hatoweza kuwafumbia macho wasanii hasa wa kike ambao wamekuwa wakivaa nusu uchi na kujidhalilisha ikiwa ni matekelezo ya tamko la Mh.rais alipokuwa akiongea na kamati ya wazazi ya CCM kuhusu maadili ya Tanzania hasa kwa upande wa wasichana.
Tarehe 7 January Naibu Waziri huyo wa habari Mh.Juliana Shonza alitoa list ya wasanii wa kike watatu ambao kwa upande wake alisema kuwa wamezidi kuweka picha chafu katika mtandao wa kijamii na wamekuwa watovu wa nidhamu na wavunjivu wa maadili kwa kiiasi kikubwa.
Wasanii hao ambao wametajwa na mh naibu waziri ni pamoja na Gigy Money, Sanchi na Pretty Kindy,hata hivyo baadha ya kutaja majina hayo mh shinza alitoa adhabu kali kwa moja ya wasanii hao ambae ni Pretty Kindy kwa kumfungia kufanya shughuli za kisanaa kwa muda wa miezi sita kwa kuacha kupost picha yoyote katika mtandao wa kijamii, kuacha kufanya show ya aina yoyote na kuacha kutoa kazi yoyote mpya mpaka adhabu hiyo itakapo isha.Agizo hilo litaanza muda mfupi tu baada ya adhabu hiyo kutolewa.
Msanii Pretty Kindy aliyefungiwa kwa muda wa miezi sita.
Lakini pia Mh.Shonza amemtaka msanii Jane Rimoy maarufu kama Sanchi kuripoti ofisini kwake mara moja kwa kosa la kuwa anaweka picha chafu katika mtandao wa kijamii , sanchi ni moja ya wasichana ambae wamekuwa wakijiachia na wako huru sana katika kuchapisha picha za utupu katika mitandao ya kijamii.
Mwanadada Jane Rimoy maarufu kama Sanchi.
Kwa upande wa Gigy Money, Mh.Shonza amesema kuwa Gigy Money hawezi kushindana na serikali kwa sababu aliambiwa afike ofisini kwake lakini amekiuka agizo hilo.
ninamtaka msanii wa bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money kufika ofisini kwangu mara moja kwa sababu alitumiwa ujumbe lakini hakujibu, ajue kuwa hawezi kushindana na serikali.
Msanii Gigy Money