Nini Amkana Ney wa Mitego Mchana Kweupe

Ikiwa ni muda kidogo umepita tangu kutokee kwa mgogoro kati ya msanii Nini na iliyokuwa menejiment yake ya zamani kwa sababu ya utovu wa nidhamu kutokana  kujiingiza katika mapenzi na msanii Ney wa Mitego,  mwanadada huyo amefunguka na kusema kuwa hajawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii huyo kwa wakati wowote tangu wajuane.

Nini aliyasema hayo alipokuwa akitambulisha wimbo wake mpya katika radio ya EATV  ambao ameshirikisha msanii Ney wa Mitego na kusema kuwa hata maamuzi ya kufanya nyimbo na Ney wa Mitego yalikuja baada ya kuingia studio na kupata vibes za studio.

download latest music    

ni kweli yaliyotokea yametokea lakini siajwahi kuwa na mahusiano na huyo kaka  na hata kufanya kazi chini ya free nation sikuwahi kuwaza lakini tu nilipata vibes za studio na zikatukutanusha na hata huu wimbo sijamuimbia yoyote  ila tu maudhui ya wimboni kama inaonekana kuwa ni dedication kwa mtu fulani.

Mwishoni mwa mwaka 2017,mtayarishaji na aliyekuwa meneja wa msanii Nini (Daxo Chali) aliweka wazi kuwa mkataba wa kufanya kazi na Nini na mwenzie hytham ulishakwisha vunjika kutokana na utovu wa nidhamu wa wasanii hao huku chanzo kikubwa ikiwa na nini kujiingiza katika mapenzi na msanii Ney wa Mitego aliyekuwa akimpa kiburi.

Hata hivo mwanadada huyo amesema kuwa pamoja na kwamba ameweza kutoa wimbo na Ney wa Mitego lakini mpaka sasa hana uongozi wowte unaomsimamia , amekuwa akifanya kazi bila kuwa na uongozi wowote kwaio kwa mwenye kutaka kufanya menejementi na yeye milango iko wazi.

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.