Idris Sultan: Wema Sepetu Hashauriki
Muigizaji wa Bongo movie na mchekeshaji Idris Sultan ameibuka na kukiri kuwa aliyekuwa mpenzi wake muigizaji wa Bongo movie mrembo Wema Sepetu amekuwa sio mtu ambaye unaweza ukamshauri.
Idris Sultan alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Wema Sepetu miaka miwili iliyopita ambapo uhusiano wao ulizidi kupata umaarufu pale walipotangaza kuwa wanatarajia kupata mtoto pamoja lakini baadae walitngaza kuwa mimba hiyo ya Wema ilitoka kwa Bahati mbaya.
Wema amekuwa Sana kwenye headlines kwa miezi hii hasa tangia afanye maamuzi yake ya kuhama chama kutoka CCM kwenda Chadems kisha kurudi tena CCM jambo lililowashangaza wengi.
Baada ya sakata hilo kutokea na kuzua maneno mashabiki wengi na watu wengi walielekeza lawama zao kwa watu wa karibu wa Wema na kuwatupia lawama kwa kutomshauri staa huyo katika maamuzi aliyoyachukua.
Kwenye interview aliyofanya na Dizzim Online Idris amefunguka haya kuhusu Wema Sepetu kurudi CCM na kurudiana na aliyekuwa mpenzi wake Luis Munana:
Kwanza kabisa kuhusu suala la kuhama vyama vya siasa I hope kuwa Wema ana Plan kwa sababu mara nyingi unakuta mastaa wanakuwa na mipango yao na mikakati lakini kwa upande wangu sidhani Kama ninaweza kufanya michezo anayofanya yeye kwa sababu sidhani kama ukiwa msanii ni salama kucheza cheza na siasa mara nyingi unaweza ukajionyesha upo upande gani ukatulia au hata ukabaki kimya na kura yako ikawa ya siri alafu ifike wakati ajue anataka nini sio unakuwa unaburuzwa kila siku lakini pia kwa mtu yeyote anayemjua Wema anajua kabisa sio mtu unayeweza kumshauri kwa lolote akakusikiliza”.