Sholo Mwamba Mbaroni Kwa Utapeli.
Msanii mkubwa na maarufu wa muziki wa singeli nchini Seif Mwinyijuma maarufu kama Sholo Mwamba asakwa na polisi kwa tuhuma za utapeli baada kutanguliziwa pesa kwa ajili ya kufanya shoo katika mkesha wa mwaka mpya katika ukumbi wa Dar Live lakini msanii huyo aliingia mitini na kutokomea na kusababisha fujo kwa mashabiki wake.
Akizungumza kuhusu tukio ilo meneja wa Dar Live, Rajab Mteta maarufu kama KP Mjomba alithibitisha kuwa alimlipa fedha nusu msanii huyo lakini hakutokea na hakutoa tarifa yoyote kuhusu kutokuja kwake katika tamasha hilo, na huku simu yake na simu ya meneja wake zikiwa hazipatikani.
Nilikubaliana na sholo mwamba afanye shoo afanye shoo katika mkesha wa mwaka mpya na hata mkataba wa fedha alizochukua nusu upo,lakini hakutokea kwa ajili ya kufanya shoo , hali hiyo imezua tafrani sana kwa mashabiki wake na kufanya tuonekane matapeli.
Mashabiki walipoona kuwa Sholo Mwamba hajatokea wakaanza kuzua tafrani, ambapo walianza kufanya fuja na kufanya uharibifu wa baadhi ya vifaa.Kitendo alichafanya sholo mwamba sio kizuri kabisa matangazo yote yalikuwa yanaonyesha kuwa atakuwepo katika shoo kama alipata matatizo alitakiwa awasiline na mimi lakini kwa ivho alichofanya ni utapeli mkubwa.
Tayari meneja huyio alishafungua kesi polisi yenye rn namba KJN/RB/12/2018