Dogo Janja Ameuanza Mwaka Kwa Kuongelea Ndoa Yake na Uwoya na Kudai Kampita Miaka 4

Mwanamuziki wa Bongo fleva Dogo Janja ameuanza mwaka mpya wa 2017 kwa kufunguka kuhusu ndoa yake na bibie Irene Uwoya au mwenyewe anavyomuita Bi. Sheila ambapo amezidi kusistiza kuwa ni mke wake halali wa ndoa kabisa.

Habari ya kufunga ndoa kati ya Dogo Janja na Irene Uwoya ni moja kati ya habari zilizokiki sana kwa mwaka 2017 kwani kuna watu wengi ambao hawakuamini kuwa Dogo Janja anaweza kumuoa muigizaji wa Bongo movie mrembo maarufu kama Irene Uwoya.

download latest music    

Pomoja na kwamba huu ni mwaka mpya umeingia lakini Dogo Janja amedai kuwa kuna watu bado hawaamini kama ni kweli yeye na Uwoya wameoana jamba ambalo amedai kuwa linamsikitisha kuwa kuna wait bado wanadhani kuwa ndoa yake ni kiki

Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa TV Dogo Janja akiwa na Made Ali wamefunguka yafuatayo kuhusiana na ndoa yake na Uwoya;

Mimi Abdulaziz Aboubakary Chende ni mume halali wa Bi . Sheila nahisi endapo huu mchongo utakuwa sio kweli nahisi watu wanichagulie adhabu alafu pia watu wengi hawaamini kuwa tumeoana kwa sababu wamezoea mtu ukiwa maarufu basi lazima uweke picha na video mtandaoni mkishikana shikana lakini sisi tumeamua ndoa yetu iwe mbali mbali na mitandao ya kijamii”.

Lakini pia baba mlezi wa Dogo Janja Made Ali amezidi kusisitiza kuwa maneno Mengi ambayo yameongelewa na yanayozidi kuongelewa kuhusiana nndoa ya Dogo Janja sio kweli has a suala la umri kuwa watu wengi wanamuita Irene kama shuga mumy jambo ambalo sio la kweli kwani Irene amempita Dogo Janja miaka minne tu.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.