Masoud Kipanya Awatoa Mashabiki Wake Wasiwasi

Msanii wa uchoraji wa vikatuni vinavyoibua hisia za mashabiki wengi kutokana na vikatuni hivyo kuwa vinaongelea maisha halisi ya mtanzania jana aliwatia wasiwasi mashabiki na watu wake wa karibu kwa kile kilichodaiwa kuwa amepotea na haijulikana wapi alipokuwa.

Majira ya saa tisa jioni habari zilisambaa katika mitandao ya kijamii kuwa Masoud Kipanya ambapo pia ni mtangazaji wa Clouds Fm amekamatwa na polisi kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kwa sababu ya uchochezi wa moja ya katuni yake aliyoichora hivi karibuni kati ya serikali na wananchi.

download latest music    

Hata hivyo baada   ya kusambaa kwa taraifa hizo mwajiri wa Masoud Kipanya, CMG-Clouds Media Group walitoa tamko katika ukurasa wao wa Instagram na kusema kuwa bado wanaangalia ukweli wa taarifa hizo na kufatilia wapi alipo na kuhaidi kuwa watatoa taarifa.

Hata hivyo ilipofika majira ya saa mbili Masoud Kipanya kupitia kurasa zake katika mitando ya kijamii aliandika kuwa ana shukuru kwa kuwa watu wanamjali na yuko salama kabisa ambapo hii iliwafanya mashabiki na watu wake wa karibu kushusha wasiwasi wao na kuamini kuwa yuko sawa.

Hata hivyo mpaka sasa jeshi la polisi alijaongea chochote kuthibitisha kuwa wao ndio waliomkamata Masoud Kipanya wala Masoud mwenyewe  hajafunguyka kuwa ni kweli alikuwa kituo cha polisi  au alikuwa amepotea kama ilivyokuwa ikisemekana.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.