Mwijaku Afunguka Mengi Juu Ya Maisha Ya Lulu Gerezani
Moja ya watu maarufu katika tasnia ya sanaa na habari anaejulikana kama Mwijaku ambae aliweza kujulikana zaidi kutoka katika tamthiliya ya mahusiano iliyokuwa ikirushwa na Clouds Mv, amefunguka na kusema mengi juu ya maisha mapaya ya msanii Lulu Michael tangu amehukumiwa kifungo chake cha miaka miwili gerezani.
Mwijaku ambae amesimulia kila kitu na hali halisi ya msanii Lulu Michael amesema kuwa Lulu kwa sasa yupo katika wakati mgumu sana kiasi kwamba hata maisha anayoishi huku gerezani hakuna ambae anaweza kuishi kama vie watu wanavyofikiria.
Mwijaku anasema kuwa Lulu Michael amekuwa akijutia kila tukio lililotokea siku ya kifo cha marehemu Kanumba na anasema kuwa anatamani hata asingpokea simu ya marehemu na kwenda nyumbani kwa marehemu usiku ule.
Hata hivyo bado Mwijaku anaendelea kusimulia na kusema kuwa Lulu anaishi maisha magumu na anasema kuwa ameshajutia na kujifunza sana kwa kila kilichotokea katika maisha yake ya nyumbani anayoishi sasa hivi. Mbali na yote msanii Lulu Michael amekuwa na wasiwasi sana hasa kuhusu maisha ya familia yake kwa sababu yeye ndie alikuwa baba na mama wa familia yake, anasikitika sana na maisha anayoishi mama yake,mdogo wake na baba yake kwa sasa kwa sababu hajui wanakula nini au kuvaa nini ilhali yeye aliyekuwa tegemezi lao hayupo tena kama zamani.
Lulu ametoa shukrani zake kwa wanaomuombea na wazidi kumuombea maana maisha ya huko sio mazuri , lakini pia anawaomba watanzania wote wamsamehe kwa kile alichokitenda ili atakapopata bahati ya kurudi uraini basi aishi maisha mapaya yenye amani.
Kwa kumalizia Mwijaku anasisitiza watu kuwa wawe na moyo ya kusameheana sana kwa kila jambo,tuwe na mioyo ya kuombeana na kukumbuka yale ya nyuma.
Mwijaku anaweza kuwa ndio mtu wa kwanza kwenda kumuona lulu michael tangu apelekwe gerezani na kuweza kuleta mrejesho wa kile alichokiona kuhusu maisha ya lulu gerezani,elizabeth lulu ichael alifungwa mwaka huu November 13, baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia ambapo alihukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani kama adhabu ya kitendo hicho.