Duma:Kuomba Omba Kunaua Sanaa ya Filamu Bongo.
Msanii wa filamu za bongo Daudi maarufu kama Duma amefunguka na kusema kuwa filamu za bongo zinakufa kwa sababu wasanii wengi wamekuwa ni omba omba na kujali maslahi yao zaidi kuliko kujali tasnia ya filamu kwa ujumla.Duma ambae kwa muda amekuwa akipiga kelele hasa kwa wasanii wenzake kuweza kujituma ili kukuza filamu bongo.
Akiongea na GPL, Duma amesema kuwa wasanii wnegi bongo wakubwa wamekuwa wakipata bahati ya kuonana na matajiri wakubwa ambao wana uwezo wa kusaidia kukuza tasnia hiyo lakini kitu cha kushangaza ni kwamba wasanii hao wamekuwa hawasema shida zinazozoikumba tasnia bali wanatoa matatizo yao binafsi na kujisaidia wenyewe, ambapo duma amewafananisha wasanii hao na ombaomba.
sanaa yetu imekufa kwa sababu kwa sababu wasanii wengi wamekuwa omba omba kwa ajili ya matatizo yao binafsi tu,ingawa wangekuwa wanaelezea matatizo ya filamu za Tanzania kwa matajiri wanaokutana nao wala filamu bongo isingekufa kabisa. Alifunguka Duma
Hivi karibuni msanii mkubwa kutoka nigeria ramsey noauh alikuja tanzania lakini alipata bahati ya kukutana na wasanii wa boingoi movies na wakafanukiwa kuongea nae na kuweza kupanga jinsi ya kuweza kuinua sanaa ya bongo.
Bado kumekuwa na changamoto sana katika kuinua tasnia ya bongo movies ingawa wapo wanaojitahidi kuinua lakini umoja wa wasanii na kujitolea kunahitajika ili kuweza kutatua changamoto hizo.