Lady Jay Dee: Utofauti wa Vipaumbele Unaweza Kutofautisha Mafanikio.
Msanii mkongwe wa kike Lady Jay Dee kutoka Tanzania amefunguka na kuongelea kwa nini inakuwa vigumu wasanii wengine kufanikiwa na wengine kufanikiwa tena akitolea mfano wake na wasanii wengine wakikke ambao wengine alianza nao muziki lakini wamekwama njiani na wengine wamekuta lakini bado wameshindwa kuendelea kufanya vizuri.
Akianza kwa kusimulia mafanikio yake baaada ya kusainiwa na kampuni moja nchini Kenya ambayo wameweza kudumu kwa zaidi ya miaka mitatu sababu menejiment hiyo imeweza ku-focus zaidi kwenye maslahi ya kwao na ya msanii pia.
Ni mkataba mzuri kwa sababu umezingatia maslahi ya pande zote mbili,ile lebo pia ni kubwa hapa afrika mashariki wanafahamu nini cha kufanya ili msanii aweze kutimiza malengo yake na ya kwao pia, kwailo ni swala la kujivunia.
Lady Jay Dee ametoa nyimbo hivi karibuni na kumshirikisha tena mpenzi wake, ambapo anasema kuwa amekuwa akimuona mwenza wake huyo akifit sana katika nafasi hizo.
nimekuwa nikimshiriksha spicy kwenye nyimbo zangu kwa sababu amekuwa aki-fit katika nafasi hiyo,ni msanii lakini pia ni mwenza wangu kwaio nitaendela kufanya nae kazi na kutoka kwenye video nyingi zijazo.
Akiongea kwa uzoefu wa kazi yake Jay Dee anasema kuwa hajui ni kitu gnai kimeweza kuwarudisha nyuma wasanii wenzake wa kike ambao alikuwa nao kwenye game miaka ya 2000 , lakini anaamini kuwa wao walikuwa na kazi nyingine nyingi zilizowafanya kushindwa kumaintain muziki.
Ni kujitambua tu na kuweka malengo na bidii, hakuna uchawi.Mimi muziki ndio kazi yangu,naenda nao kulingana na mahitaji ya soko,siwezi jua kwanini wao walikwama inawezekana hiyo sio kazi yao namba moja.Tunatofautiana maisha kila mtu ana kipaumbele chake.
Jay Dee anasema kuwa imekuwa ni changamoto kubwa sana wanapokuja wasanii wachanga na kujikuta wakifanya nao ushindani sokoni lakini pia anafurahia kitu hicho kwa sababu wanamfanya apate changamoto na kujikuta akifanya vizuri na kuwa mpya kila siku.
Mimi nimechagua kazi ya muziki kwa sababu kila kitu napata huku,kwaio ni lazima niwe makini na kazi hiyo, najiona ndio kama naanza.nafurahi sana ninapoona wasanii wachanga wanapokuja na kutukuta na kutupa changamoto.