Wasanii Walionja Selo Mwaka 2017.
Ni majaribu mengi binadamu wanakutana nayo, mengine Mungu anampa mtu ili kumpima na kuona kama anaweza kuyahimili kwa kishindo gani, lengo kubwa hapa ni kumuhaibisha shetani na njia zake,wakiwa kama wasanii yapo mengi hutokea kwao lakini haifanyi kuacha kuendelea kukonga nyogo ya mashabiki kwa sababu wao dfio wanakuwa wamekuweka hapo ulipo.
Mwaka 2017, unakaribia kuisha na kila mtu anaweza kusema lake kwa kumshuuru Mungu kuumaliza salama punde mwaka utakapokuwa umeisha lakini hakuna anekosa cha kusimulia tena hasa anapokutana na tukio kubwa ambalo labda kwa namna moja ama nyingien imeweza kubadili maisha yake kwa ujumla au kwa kiasi fulani.
Hawa wafuatao ni baadhi ya wasanii ambao endapo watapata fursa ya kuongelea yaliyowakuta 2017, basi hawatasita kuongelea kitendo cha wao kulala selo kwa mwaka 2017, hii inaweza kuwa ni historia yAo isiyo weza kufutika kamwe.
NEY WA MITEGO
Ney wa mitego alikamatwa na kuwekwa ndani mwanzoni mwa mwaka huu baaada ya kuachi wimbo wake wa wapo ambao ulitafsiriwa kuwa ulikuwa unalengo la kuwakasfu viongozi waliopo serikalini.alikaa ndani kwa muda wa siku mbili.
ELIZABETH LULU MICHAEL.
Mpaka muda huu bado yupo gerezani, kesi yake ya mauaji ndio iliompeleka huko, lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la kuua bila kukusudia.Akiwa msanii mwenye umri mdogo laini amepitia meng magumu, hakika mwaka huu ni mwaka mgumu kwake na familia yake.
WEMA SEPETU.
Alijikuta akiingia matatani baada ya pilika pilika z akutafut watumiaji wa madawa ya kulevya mkumbo ambao uliwanasa wasanii wengi sana katika tasnia ya filamu na muziki pia.alitok selo lakini kesi yake bado inasikilzwa mahakamani.
VANNESA MDEE
Ni moja ya wasanii wakubwa wakikie na wanaofanya vizuri tanzania na nje ya tanzania, alijikuta lock-up baada ya kutajwa katika list ya wasanii wanaotumia unga mapema mwaka huu katika kampeni iliyoanzishwa na mkuu wa mkoa.
Wasanii wengine ni pamoja na Recho, T.I.D,Petit man, na video quen Tunda.tunaamini mpaka mwaka unaisha hakuna atakaekutana na tukio baya tena.