Mama Ashura Aendelea kula Sahani Moja Na Kiba
Moja ya wachekeshaji wanaofanya vizuri kutoka kundi la Timamu ambae amekuwa akimkosoa sana Alikiba kutoakana kazi zake za muziki anazofanya anaejulikana kwa jina la usanii kama Mama Ashura wikiendi hii alifunguka tena na kusema kuwa hatokaa akome kumkosoa Alikiba kama anafanya vibaya katika kile anachokifanya na kwamba kama itatokea siku akifanya vizuri pia hatoacha kumsifia.
Mama Ashura alishawahi kufikia hatua ya kurushiana maneno na mdogo wake wa kike na msanii huyo alikiba anaejulikana kwa jina Zabibu Kiba kuhusu kaka yake, hata hivyo Alikiba amekuwa kimya kwa kipindi chote ambacho mwanamama huyo amekuwa akimkosoa.
Akiongea katika mahojiano na mwandishi mmoja wa habari wikiendi iliyopita walipokuwa katika uzinduzi wa filamu ya FROM NIGERIA ,, Mama Ashura alipoulizwa kama ataweza kuhudhuria endapo Alikiba atakuwa anatambulisha wimbo mpya, mama huyo alijibu kuwa kuhudhuria atahudhuria na kumkosoa bado atamkosoa tu kwani Alikiba ni nani mpaka asiambiwe.
Ofcourse angekuwa ni Alikiba ningekuja na ingekuwa nzuri ningesema na ingekuwa mbaya pia ningesema vilevile,kwani kiba nani , kwanini asiambiwe, ni lazima tujifunze kupitia wengine wanapotukosoa ,kila mara , na kama yeye ataona kibaya cha kwangu basi aseme tu , tunamchana tu. Alisema Mama Ashura.
Alikiba amekuwa moja ya wasanii wanaosemwa sana katika mitandao ya kijamii lakini siku zote amekuwa sio mtu wa kujibu tuhuma za mashabiki badala yake hufanya vitu vinavyomuhusu.hii haitakuwa mara ya kwanza kwa mama ashura kumsema Alikiba lakini msanii huyo hunyamaza kimya kama vile haoni kinachoendelea.