Kuja Kwa Ramsey Nouah Kuliamsha Kilio Kwa Mama Kanumba.
Mwanamaigizo maarufu kutoka Nigeria Ramsey Noauh alikuwa Tanzania hivi karibuni ambapo alishirikiana na wasanii kama Idris sultani na mwana mitindo na mrembo mwanaharakati Jokate Mwegelo katika kuogoza kongamano la vijana lililofanyika Chuo Kikuu Cha UDSM kwa ajili ya kuongea na vijana jinsi ya kusimama na kujikwamua kupitia tasnia hiyo.
Lakini msanii Ramsey hakusita kwenda na kudhuru kaburi la aliyekuwa rafiki yake na msanii mwenzie amabe walifanya kazi pamoja siku za nyuma za uhai wake kabla ya kukutwa na umauti wake , marehemu Steven Kanumba.Kwa masikitiko makubwa msanii huyo alionekana kuguswa sana na kifo hicho ukizingatia walikuwa tayari walishapanga mengi katika kukuza na kufanya kazi pamoja za sanaa.
Kwa kushirikiana na wasanii wengine na wadau wengine wa sanaa nchini Ramsey Nouah aliambatana na familia ya Kanumba akiwepo mama na mdogo wake marehemu mpaka kwenye kaburi la Kanumba, ambapo kilio cha msiba huo kilikuwa kama kinaanza upya kwa familia ya Kanumba hasa mama mzazi ambae alikuwa akionekana kulia muda wote.
Hata hivyo Ramsey alionyesha kufikwa kwake na msiba huo na kusema kuwa
steven kwa mara ya mwisho tulikuwa tukizungumza wote ulikuwa hai lakini leo ninazungumza na wewe ukiwa umelala hapa kwenye mchanga hujitambui, kwangu ni zaidi ya msiba na kweli nimeshindwa kuhimili jambo hili.Najua uko ulipo unamia sana na ukizingatia unaona na unajua kabisa tasnia ya muvi Tanzania inakufa.Alizungumza Ramsey alipokuwa amesimama mbele ya kaburi la Kanumba huku akizungumza maneno hayo yaliyoibua hisia za waliokuwepo hasa mama wa marehemu.