Mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa Freemason Afrika Mashariki yachomwa moto jijini Dar es Salaam (Video)
Freemasons wamekuwa wakitajwa kwenye kila aina ya minong’ono. Kuna wale wanaosema kuwa dini hilo ni la kishetani – eti wale ambao wanataka kupata utajiri na kuwa watu wenye nguvu ndo wafwasi wa Freemason.
Aliyekuwa kiongozi wa Jumuiya ya Freemason Tanzania na Afrika Mashariki, Sir Jayantilal Keshavji ‘Andy’ Chande alifariki Aprili 7 mwaka huu jijini Nairobi, Kenya.
Mwili wa mwendazake ulichomwa moto mpaka kubaki majivu Aprili 10 katika sherehe maalum iliyoandaliwa Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.
Mwili huo uliteketezwa kwa moto kupitia ibaada iliyofanyika kwenye nyumba maalumu inayotumika kama sehemu ya maziko ya waumini wa dini ya Hindu.
Tazama video hapo chini: