Wastara Afunguka Siri Ya Kutokukata Tamaa Baada Ya Kupata Matatizo
Mwanadada msanii mkongwe Tanzania Wastara Sajuki ,ambae alipitia magumu mpaka hapa alipofikia amefunguka na kuelezea maisha ya ke na magumu aliyoyapitia tangu alipopata ajali yake yeye na mumewe na baadae mume wake kuumwa na kulazwa kwa muda mrefu sana na hatimaye kuaga Dunia.
Wwanadada huyo ambae ni muigizaji, lakini pia ni mwimbaji na mjasiriamali lakini kwa sasa pia ameonyesha uwezo wake mkubwa wa kuingia katka siasa na kufanya vizuri . Wastara ameamua kuongea na kuwashauri wanawake wengine wasikate tamaa baada ya kupata matatizo hayo kwa sababu yeye pamoja na kupata matatizo hayo hakuwahi kukata tamaa bali iliendelea kumpa chachu ya maendeleo.
Wastara anaeleza kuwa kipindi anaanza sanaa tayari alikuwa ni mfanya bashara lakini hakukata tamaa na kuacha biashara yake kwa sababu alijua vitu vyote viwili akiweza kuvimudu basi ataweza kufanya vizuri.Akiendelea kuongezea kuhusu mahangaiko yake Wastara anasema
kweli tangu nimepata ajali matatizo mengi sana yalijitokeza,unajua siku napata ajali ndio ilikuwa siku ambayo nilitakiwa nikanunue gauni langu la harusi.kwaio mipango mingi ilivurugika na hata nilipokatwa mguu nilifunga ndoa baadae mume wangu akanza kuuumwa na nilingaika nae sana lakini yote kheri namshukuru Mungu.
Kwangu mimi sijioni kama mlemavu kabisa, na ndio maana unaona ninaigiza na na kushiriki katika mambo mengine mengi ya mikakati ya kimaisha ikiwepo siasa na jamii , kwaio nawasihi waache kulitafuta tatizo lao na badala yake watafute namana na suluhu ya kukabiliana na matatizo hayo.
Hata hivyo Wastara ambae hivi karibuni ametoa wimbo unaowahamasisha wanawake amesema kuwa ameamua kuongea na wanawake wenzie ili kujikita katika kupambana na ndoto zao , lakini pia nyimbo hiyo sio kwa wanawake tu bali hata kwa wanaume ambao wanakata tamaa mapema waaachena huo wimbo unawahusu.
Wastara anaongezea na kusema kuwa wanawake wengi wanakuwa na visingizo kuwa wanashindwa kuanzisha biashara kwa kisingizio cha kuwa na mitaji , lakini anachowaambia ni kuwa kitu kikubwa nai kuwa na wazo zuri la biashara kwanza.